Genesis 10:21-29

Wazao Wa Shemu

21 aShemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

22 bWana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23 cWana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24 dArfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
27 eHadoramu, Uzali, Dikla, 28 fObali, Abimaeli, Sheba, 29 gOfiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
Copyright information for SwhNEN